Wednesday 25 March 2015

Tutafika kweli kwenye uhuru tuutakao


Kila mwaka mei tatu waandishi wa habari duniani kote hukumbuka siku yavyombo vya habari , siku hii ni mahususi kwa kuziangalia changamoto na mafanikio katika tasnia ya habari nchini Tanzania.

Miaka minne iliyopita siku hii ya waandishi iliingia dosari kubwa mno baada ya mwandishi wa habari aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi mkoani iringa Daudi Mwangosi kuuwa katika mazingira tata na jeshi la polisi.

Hapo ndipo jitihada zikaongezwa katika kuzipigania haki za waandishi wa habari nchini Tanzania lakini kuna shida kubwa sana katika utendaji wao zinazosababishwa na kutokuwapo na uhuru wa vyombo vya habari wa kiwango cha kutosheleza
Tafsiri ya Uhuru wa vyombo vya habari inaelezwa pale   vyombombo vya habari vinapoweza kutoa taarifa ama ripoti zenye ukweli mtupu kwa masuala ya kijamii bila kujalisha ni mema au la kwa ajili ya faida ya taifa
Kwa mujibu wa kituo cha stan hope vyombo vya habari nchini Tanzania havikuwa na chachu ya kuibua mambo mazito kwa takribani miaka kumi iliyopita sababu inayotajwa ni kwamba uwepo wa chama kimoja kinachoongoza nchi kuwa na umiliki wa magazeti na redio ambazo hazikuwa zikitumika kwa ajili ya maslah ya taifa moja kwa moja bali kwa makusudi ya waliovianzisha

Leo hii nchi ya Tanzania inafurahia zaidi ya magazeti 400 na kwa kiwango kikubwa yanafikisha ujumbe wake kwa kutumia lugha ya taifa ya kishwahili. Ingawa kiwango kikubwa cha magazeti haya yapo jijini dar es salaam lakini pia tuna takribani zaidi ya vituo vya luninga 10, na kiwango kikubwa sana cha redio haya ni mafanikio ya kujitamba.

Ingawa katiba ya nchi ya Tanzania inatoa fursa ya uhuru wa vyombo vya habari bado kuna changamoto ya kubanwa kwa maeneo mengi ya kazi za kiuandishi takribani  kuna sheria 17 ambazo zinawabana waandishi ama vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa umakini

Kumekuwapo na taarifa kadhaa za serikali kuendelea kufifungia vyombo kadhaa hususani magazeti na wavuti pindi wanapokuwa na habari zenye uchambuzi wa kuikosoa serikali kwa kiwango kikubwa

Madhalani Sheria ya usalama wa taifa inatoa ruhusa kwa serikali kutoa adhabu kwa taarifa zozote za kiuchunguzi zinazoweza kugusia taarifa ambazo zinaitwa za siri

Hata hivyo hakuna mshikamano dhabiti baina ya waandishi wa habari wa Tanzania na hata hawana umoja unaoweza kusimama kidete kutetea maslah yao kinachofanyika ni kumshukuru mungu walau kuna amani lakini waandishi wa habari wana budi ya kutafuta mbinu ya kuwaweka umoja dhubuti utakaoweza kuwasimamia maslahi yao.

Changamoto kadhaa bado zinawakumba waandishi, ufinyu wa maarifa na elimu duni inawakosesha haki hata pale wanapokuwa na haki ya kupata taarifa mbalimbali ingawa mara kadhaa idara mbalimbali za serikali zimeripotiwa kuwa mbele katika kuwanyima waandishi haki ya kupata taarifa.

Taarifa hii ni uchambuzi wangu kutoka kwenye mtandao









No comments:

Post a Comment