Kila mwaka mei
tatu waandishi wa habari duniani kote hukumbuka siku yavyombo vya habari , siku hii ni mahususi kwa kuziangalia changamoto na
mafanikio katika tasnia ya habari nchini Tanzania.
Miaka minne
iliyopita siku hii ya waandishi iliingia dosari kubwa mno baada ya mwandishi wa
habari aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi mkoani iringa Daudi Mwangosi kuuwa katika mazingira tata na jeshi la
polisi.
Hapo ndipo
jitihada zikaongezwa katika kuzipigania haki za waandishi wa habari nchini
Tanzania lakini kuna shida kubwa sana katika utendaji wao zinazosababishwa na
kutokuwapo na uhuru wa vyombo vya habari wa kiwango cha kutosheleza
Tafsiri ya
Uhuru wa vyombo vya habari inaelezwa pale
vyombombo vya habari vinapoweza kutoa taarifa ama ripoti zenye ukweli
mtupu kwa masuala ya kijamii bila kujalisha ni mema au la kwa ajili ya faida ya
taifa
Kwa mujibu
wa kituo cha stan hope vyombo vya habari nchini Tanzania havikuwa na chachu ya
kuibua mambo mazito kwa takribani miaka kumi iliyopita sababu inayotajwa ni
kwamba uwepo wa chama kimoja kinachoongoza nchi kuwa na umiliki wa magazeti na
redio ambazo hazikuwa zikitumika kwa ajili ya maslah ya taifa moja kwa moja
bali kwa makusudi ya waliovianzisha
Leo hii nchi
ya Tanzania inafurahia zaidi ya magazeti 400 na kwa kiwango kikubwa yanafikisha
ujumbe wake kwa kutumia lugha ya taifa ya kishwahili. Ingawa kiwango kikubwa
cha magazeti haya yapo jijini dar es salaam lakini pia tuna takribani zaidi ya
vituo vya luninga 10, na kiwango kikubwa sana cha redio haya ni mafanikio ya
kujitamba.
Ingawa
katiba ya nchi ya Tanzania inatoa fursa ya uhuru wa vyombo vya habari bado kuna
changamoto ya kubanwa kwa maeneo mengi ya kazi za kiuandishi takribani kuna sheria 17 ambazo zinawabana waandishi
ama vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa umakini
Kumekuwapo
na taarifa kadhaa za serikali kuendelea kufifungia vyombo kadhaa hususani
magazeti na wavuti pindi wanapokuwa na habari zenye uchambuzi wa kuikosoa
serikali kwa kiwango kikubwa
Madhalani Sheria ya usalama
wa taifa inatoa ruhusa kwa serikali kutoa adhabu kwa taarifa zozote za
kiuchunguzi zinazoweza kugusia taarifa ambazo zinaitwa za siri
Hata hivyo
hakuna mshikamano dhabiti baina ya waandishi wa habari wa Tanzania na hata
hawana umoja unaoweza kusimama kidete kutetea maslah yao kinachofanyika ni
kumshukuru mungu walau kuna amani lakini waandishi wa habari wana budi ya
kutafuta mbinu ya kuwaweka umoja dhubuti utakaoweza kuwasimamia maslahi yao.
Changamoto
kadhaa bado zinawakumba waandishi, ufinyu wa maarifa na elimu duni inawakosesha
haki hata pale wanapokuwa na haki ya kupata taarifa mbalimbali ingawa mara
kadhaa idara mbalimbali za serikali zimeripotiwa kuwa mbele katika kuwanyima
waandishi haki ya kupata taarifa.
Taarifa hii ni uchambuzi wangu kutoka kwenye mtandao